Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA, taasisi nyingine 32 sasa kufanya kazi jengo moja

81943 Pic+tpa TPA, taasisi nyingine 32 sasa kufanya kazi jengo moja

Mon, 28 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na taasisi nyingine 32 zimeanza kufanya kazi katika jengo moja ili kuongeza ufanisi.

Amesema lengo la kufanya hiyo ni kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu hasa katika mchakato wa utoaji wa mizigo bandarini kwa saa 24.

Kamwelwe ametoa kauli hiyo leo Jumapili Oktoba 27, 2019  alipokutana na watendaji wa TPA na wa taasisi hizo zikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Shirika la Reli Tanzania (TRC).

“Tutafanya kazi kwa pamoja katika jengo moja kwa saa 24 ili kurahisisha huduma kwa mteja. Kama kuna TPA, TRA na  TBS (Shirika la Viwango) mteja atatoka meza moja kwenda nyingine, mfumo huu utaratibu utoaji wa mizigo utakwenda haraka.”

“Lengo jingine la mkutano ni kuangalia kama TPA, taasisi hizo 32 zimeanza kufanya kazi pamoja kwa sababu bado kuna malalamiko machache ninayoyapokea,” amesema.

Amesema walichokibaini katika utendaji kazi wa  taasisi hizo ni kila mtu kufanya kazi kivyake, “hata utoro unaweza kutokea, hivyo nimempa jukumu katibu mkuu wa Uchukuzi kuunda kamati maalumu kuangalia mwenendo wa watendaji hao wanapokwenda kazini ikiwemo kuweka rekodi zao.”

Pia Soma

Advertisement
“Tumejadili mengi na tumekubaliana kukutana mara moja kwa mwezi na kila mtu amezungumza changamoto anazokutana nazo. Tunataka kuziondoa changamoto hizi na tusingependa kuona mteja akilalamika kwa sababu zenye ukweli.”

Chanzo: mwananchi.co.tz