Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA na Dangote waingia makubaliano ya kibiashara

DILT Sasa urari wa biashara kati ya TPA na Dangote utaongezeka kufikia 43%

Wed, 16 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeingia makubaliano ya kibiashara na kampuni ya uzalishaji saruji ya Dangote, yatakayowezesha usafirishaji wa bidhaa zinazozalishwa na kusimamiwa na kiwanda hicho kuongezeka kutoka tani elfu 15 kwa mwezi hadi kufikia tani elfu 43 kwa mwezi.

Akizungumza mkoani Mtwara kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Meneja Masoko wa mamlaka hiyo Lydia Mallya amesema kuwa awali kampuni ya Dangote ilikuwa inasafirisha bidhaa kama saruji kwa njia ya barabara kwenda mikoa mbalimbali ikiwaa ni pamoja na Dar es Salaam na Kigoma.

Mallya amesema makubaliano hayo yataongeza ufanisi wa bandari ya Mtwara kwa kuvutia shehena nyingi zaidi ziweze kupita katika bandari hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania kwa hatua hiyo ambayo amesema itashusha bei ya saruji ndani na nje ya nchi, kufungua fursa za kiuchumi na uwekezaji kwa mkoa huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live