Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA kushirikiana na DP World

Dp World Somaliland Somalilanddd.png TPA kushirikiana na DP World

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imejipanga kushirikiana na kampuni ya DP World ili kuongeza ufanisi wa huduma za kibandari na kuwezesha ongezeko la meli na shehena katika Bandari ya Dar es Salaam.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Juma Kijavara ametoa kauli hiyo mkoani Dar es Salaam wakati wa kikao cha wadau wa bandari na sekta ya uchukuzi kuhusu mipango mkakati uliowekwa wa namna ya kushirikiana na wawekezaji wa nje katika kutoa huduma kwenye bandari hiyo ya Dar es Salaam.

Kijavara amesema uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam utaleta ongezeko kubwa la meli na shehena, na hivyo kuhitaji wadau waliojipanga vema kukabiliana na ongezeko hilo kwa ufanisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live