Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA kupewa bilioni 35 kila mwezi

Pesa Fedhaddd TPA kupewa bilioni 35 kila mwezi

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imetakiwa kuipatia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) shilingi Bilioni 35 kila mwezi kutoka kwenye makusanyo kwa kuwa mapato yote yanayopatikana kutoka kwenye tozo za gati huchukuliwa na Serikali bila TPA kubakiziwa chochote.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu Selemani Kakoso akisoma taarifa Bungeni jijini Dodoma kuhusu shughuli za kamati hiyo kwa mwaka 2023 amesema utaratibu wa kukusanya fedha zote unaiminya TPA kufanya maboresho ya miundombinu katika magati hata kuipunguzia Serikali kupata mapato zaidi.

Aidha, taarifa hiyo imesema yapo malalamiko kuhusu ufanisi wa TPA kutokana na kutokamilika kwa mifumo ya TEHAMA inayosoma kwa kuunganisha wadau pamoja na hali isiyoridhisha ya miundombinu inayowezesha uchukuzi wa shehena kutoka bandarini, hali inayoweza kusababisha mlundikano wa shehena bandarini na kukwama kwa azma ya uboreshaji wa huduma zinazotolewa na Mamlaka hiyo.

Kutokana na malalamiko hayo, Bunge limeitaka TPA kuongeza kasi ya kuboresha miundombinu ya barabara na njia za reli zinazoingia na kutoka Bandari ya Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live