Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA, TRA kuimarisha ushirikiano kuongeza ufanisi

TRA TPA TPA (600 X 394) TPA, TRA kuimarisha ushirikiano kuongeza ufanisi

Wed, 28 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa jitihada zake kubwa za kuimarisha utendaji wa Sekta ya Bandari nchini, ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Pongezi hizo zimetolewa na Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda, alipotembelea Bandari ya Tanga akiwa ameongozana na Mwenyeji wake, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa, na kushuhudia mageuzi makubwa yaliyofanywa katika bandari hiyo kufuatia uwekezaji uliofanywa kwenye miundombinu na vitendea kazi bandarini hapo.

Kamishna Mkuu Mwenda amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili katika kuongeza ufanisi wa huduma zao na mchango wao katika maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa, ameipongeza TRA kwa ushirikiano uliopo kati yao na kuahidi kuimarisha zaidi ushirikiano huo, hususan katika eneo la matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuhakikisha usahihi wa taarifa za shehena na tozo zinazostahili kutozwa.

Aidha, viongozi hao walipata fursa ya kutembelea bandari za Pangani na Sahare, kujionea utoaji huduma, na kujadiliana namna bora ya kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato katika bandari hizo ndogo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live