Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA, EACOP wasaini mikataba ujenzi bomba la mafuta

TPA EACOP.png TPA, EACOP wasaini mikataba ujenzi bomba la mafuta

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeingia mikataba mitatu na East African Crude Oil Pipeline Limited (EACOP), kwa ajili ya kuridhia kutumika kwa Bandari ya Tanga wakati wa utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani, Tanga Tanzania.

Mikataba hiyo mitatu inayohusisha kukodi eneo la kujenga miundombinu ya kuhifadhia mafuta, imesainiwa jana Jumanne, Machi 26, 2025 Kata ya Sojo, Wilaya ya Nzega mkoani Tabora mbele ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko.

Mikataba hiyo kwa upande wa TPA imesainiwa na Mkurugenzi Mkuu, Plasduce Mbossa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa mamlaka hiyo, Ernest Mangu.

Lingine lililomo kwenye mkataba huo ni kutumia eneo la maji katika Bandari ya Tanga ambapo TPA imetoa sehemu ya gati mita 200 kwa mkandarasi wa mradi Kampuni ya BBN Ltd kwa ajili ya kuegesha vyombo vinavyotumika kupokea na kupeleka vifaa mbalimbali vya ujenzi wa gati maalumu (Jetty) la kupokelea mafuta ghafi.

Mikataba hiyo imeelezwa ni muhimu katika utekelezaji wa mradi wa EACOP hususani sekta ya usafirishaji majini, na kwa mujibu wa sheria TPA imepewa jukumu la kusimamia maeneo yote ya fukwe na mwambao kwa ajili ya shughuli za kibandari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live