Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPA, Dangote waingia makubaliano kusafirisha saruji

Tpa Pic Data TPA, Dangote waingia makubaliano kusafirisha saruji

Wed, 16 Mar 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imeingia makubaliano na Kiwanda cha Saruji Dangote ya kusafirisha saruji kupitia Bandari hiyo ambayo ina uwezo wa kusafirisha zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka.

Akizungumza leo Jumatano Machi 16, 2022 baada ya makubaliano hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema kuwa kwasasa Bandari ina uwezo wa kuhudumia zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka, mafuta lita milioni 6 kila mwezi na makaa ya mawe tani 30,000 kila mwezi.

“Dangote ni kiwanda kikubwa kimekuwa msaada mkubwa katika uzalishaji wa saruji nchini uwepo wake kwetu ni faraja ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samiah Suluhu na haya ni moja kati ya mafanikio makubwa kwake baada ya bandari kuongezewa uwezo wa kusafirisha shehena kubwa zaidi”

“Ongezeni bidii ya kufanya kazi tunaompango wa kuongeza uzalishaji wa korosho ili tuweze kutumia bandari hii kwaajili ya usafirishaji niwahakikishiei kuwa mkoa uko tayari kuendelea kushirikaina na dangote ili muweze kufanikisha lengo lenu la kuongeza uzalishaji wa sarufui ili mtwara na nchi kwa ujumla ziweze kufanikiwa”

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Lyidia Malya amesema kuwa kiwanda hicho kimekuwa kikitumia bandari hiyo kusafirisha shehena za saruji kwenda Zanzibar, Comoro na Msumbiji ambapo makubaliano hayo yataongeza wigo wa usafirishaji wa saruji katika maeneo mbalimbali duniani.

 “Zipo faida kubwa kwa bandari ya Dar es salaam, Tanga na Mtwara ambapo kutakuwa na ongezeko la usafirishaji wa shehena  mbalimbali na kutunza miundombinu ya barabara ambapo utachagiza kufungua wigo wa biashara katika ushoroba wa Mtwara na kufanya bandari kupata fedha na kuongeza ajira  kwa watanzania” amesema Malya

Kwa upande wake Meneja wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Nchini Tanzania, Abdullahi Baba amesema kuwa wamekuwa wakipata shida kuingia katika ushindani wa kibiashara na viwanda vingine vya kutengeneza bidhaa hiyo nchini kutokana na kusafiri umbali mrefu kuipeleka sokoni.

“Unajua saruji ya Dangote soko kubwa liko nje ya mkoa wa Mtwara ndio maana unaweza kuona tunakwenda Dar es Salaam   hadi Kigoma wakati mwingine usafiri unakuwa ni changamoto kusambaza saruji yetu lakini sasa matumizi ya bandari yatasaidia na kurahisisha kazi zetu”  amesema Baba

Chanzo: www.mwananchi.co.tz