Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa amesema Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikiendeshwa kwa ubora kwa kuhudumia wateja na wadau hadi kutoka nchi jirani, hivyo kutokana na kuwa na jukumu hilo, bandari hiyo ilijiwekea malengo ya utoaji huduma kuanzia mwezi Julai hadi Desemba 2023 ambapo katika kutoa huduma hizo, bandari imefanya zaidi ya malengo yake.
Kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2023 Bandari ya Dar es Salaam imehudumia takribani meli 979 kati ya meli 792 zilizokuwa zimekusudiwa, ambapo ni zaidi ya malengo yaliyokusudiwa.
Amesema bandari hiyo imehudumia abiria takribani milioni 1 kati ya 900,000, makasha 990,000 kati ya lengo la kuhudumia makasha 500,000, huku mizigo ikiwa ni tani milioni 17.2 kati ya tani milioni 15.6 zilizokusudiwa.
Amesema hayo leo katika mkutano wa TPA na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa ufanisi wa bandari hiyo unachangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi wa nchi.