BARAZA la Taifa la Biashara (TNBC) limesema Serikali ya Awamu ya Sita imeboresha mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji.
-
Katibu Mtendaji wa TNBC, Dk Godwill Wanga amesema kumekuwa na maboresho yakiwamo ya sera kuondoa tozo na ukiritimba uliokuwa unakwamisha ustawi wa biashara na uwekezaji nchini.
-
Alisema hayo Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ambayo TNBC imepata.
-
Alisema katika kipindi cha miaka mitatu, Rais Samia Suluhu Hassan ameifungua nchi kiuchumi ikiwemo kuimarika kwa ushirikiano na uhusiano kati ya sekta binafsi na umma. Imetekeleza pia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (Mkumbi) ili kuvutia uwekezaji na kukuza biashara nchini.
-
Dk Wanga alisema kwa kuongozwa na Rais Samia, TNBC imeimarisha mabaraza ya biashara ya mikoa na mabaraza ya biashara ya wilaya na imetatua changamoto zilizowakabili wafanyabiashara.
-