Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TNBC kuzipa thamani bidhaa za Mbao

Bidhaa Za Mbao TNBC kuzipa thamani bidhaa za Mbao

Sat, 28 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Kitaifa la Biashara (TNBC)linafanya mradi ambao umebuniwa kwaajili ya kukuza uzalishaji na utngenezaji wa bidhaa zitokanazo na miti.

Kupitia kikundi cha Kuhifadhi Misitu (FWG), TNBC imeandaa mkakati maalumu wa kukuza na kuzitangaza bidhaa za mbao nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa TNBC Dr.Godwill Wanga wakati wa mkutano wa nane na Kikundi cha kuhifadhi misitu (FWG) alisema ni muhimu kuziongozea thamani bidhaa zitokazo na misitu kwahiyo zina jukumu muhimu katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania.

Dk Wanga alisema TNBC ilipewa jukumu la kuandaa mkakati wa kuboresha bidhaa za misitu kwa kushirikiana EWP wakati wa mkutano wa 12 wa TNBC, ambao uliongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Alisema sekta ya misitu ina faida kubwa, ikiwa ni pamoja na kutengeneza nafasi za ajira kwa Watanzania na kuongeza mapato ya fedha za kigeni nchini kupitia usafirishaji wa bidhaa za misitu kwenda nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live