Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TMA yawatahadharisha wakulima mabadiliko Tabianchi

Kilimo TMA yawatahadharisha wakulima mabadiliko Tabianchi

Wed, 8 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ongezeko la joto nchini limeleezwa kupunguza uzalishaji wa zao la viazi mviringo katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa kipindi cha miaka ishirini ijayo kutokana na mabadiliko ya tabianchi hususan mvua chache na ukame.

Meneja wa  Huduma za Hali Hewa ya Kilimo kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Isack Yonah amesema leo Jumatano, Juni 8, 2022  mkoani hapa kwenye kikao kilichohusisha  wadau wa kilimo, makampuni ya pembejeo, watafiti na maofisa kilimo kilichoratibiwa  na Mradi  wa Craft kwa udhamini wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi.

Yonah amesema kuwa mabadiliko ya tabianchi yataleta athari kubwa ya uzalishaji kwa kipindi cha miaka ishirini ijayo. Hivyo ni vyema  watafiti, maofisa kilimo na wadau kushirikiana ili kusaidia wakulima kuzalisha mazao mbadala tofauti na viazi mviringo

''Kikao hiki kitatoka na majibu ya nini kifanyike katika kusaidia Serikali na wakulima wanaozalisha mazao ya kilimo cha biashara kwa kutoa elimu ya kilimo  mbadala ili kuwaepusha na hasara kutokana na mabadiliko ya tabia nchi,'' amesema.

Ameongeza kuwa TMA imekuwa ikifanya utabiri wa mara kwa mara kuangalia hali ya kilimo na mazao kwa miaka ijayo hivyo ni wakati kwa wakulima kubadilishwa kimtazamo mapema kabla athari kujitokeza kwa kuzalisha mazao yanayo himili ukame.

 Ofisa Kilimo Mwandamizi kupitia Mradi  Craft wa  kilimo himilivu cha mazao, Godyfrey Kabuka amesema wamelazimika kukutana na  wadau hususan wakulima lengo la kutoa elimu ya athari ya  mabadiliko ya hali ya hewa katika uzalishaji na  kutoa  fursa za kilimo mbadala kinacho himili ukame

Amesema mradi huo unatekelezwa kwa miaka mitano ambao unawakutanisha wadau kueleza mabadiliko kwenye sekta ya kilimo na  kutoa elimu ya athari katika uzalishaji wa  viazi mviringo na kutoa  fursa zilizopo kwenye mnyororo wa thamani

''Nishauri watafiti kuja na mpango wa mbegu bora ambazo zitastahili ukame lengo likiwa ni kuwawezesha wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuzalisha mazao yanayokabiliana na ukame,''amesema.

Mkulima wa viazi, Stella Mwamakula amesema  upungufu wa mvua umeathiri uzalishaji  katika baadhi ha maeneo nchini ikiwa ni pamoja na gharama za mbolea kutoka Sh40,000 mpaka 120,000 na kwamba hali ya kupungua kwa uzalishaji kuna wakatisha tamaa na kuomba elimu ya kilimo mbadala kipewe kipaumbele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live