Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TIRDO yaja na maabara ya kupima ngozi

Kupima Ngoziiii (600 X 366) TIRDO yaja na maabara ya kupima ngozi

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), limeanza kufanya uhakiki wa bidhaa za ngozi ili kukidhi viwango vya ushindani kwenye masoko ya kimataifa kwa bidhaa za Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa TIRDO Prof. Mkumbukwa Mtambo ameiambia TBC Online kuwa, vifaa vya kisasa vilivyosimikwa kwenye maabara ya ngozi vina uwezo wa kuhakiki ubora wa bidhaa hizo kwa asilimia mia moja.

Ameongeza kuwa, Maabara hiyo ina uwezo wa kupima ngozi na bidhaa zake na kujua viwango mbalimbali vya utimamu kwenye bidhaa hizo.

Prof. Mtambo amewataka wazalishaji na wajasiriamali kuitumia maabara hiyo kuhakiki ubora wa bidhaa za ngozi kabla ya kuzipeleka kwenye masoko mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live