Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TIRA, NIC, IFAD kuja na mpango bima ya kilimo

Ca4e87d8fe53c3ce55f85b2de604b031 TIRA, NIC, IFAD kuja na mpango bima ya kilimo

Tue, 25 Jan 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) kwa kushirikiana na Shirika la Bima la Taifa (NIC) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD) wamepanga kubuni mpango wa Bima ya Kilimo (National agriculture Scemee) kwaajili ya kuwafikia wakulima, wavuvi na wafugaji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 24, 2022 katika Ofisi za NIC, jijini Dar es Salaam Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Baghayo Saqware amesema hatua hiyo itaongeza wigo mpana kwa kuwafikia watanzania wengi.

“Tumeona mpango lazima uanzie NIC ili kuwafikia watu wengi zaidi. Tumeona kila Mtanzania ambaye anafanya shughuli zake za kilimo, aweze kupata kinga ya shughuli zake za kilimo,” amesema Baghayo.

Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Jackline Motcho amesema wafugaji na uvuvi wameridhia kushirikiana na Serikali kwenye suala hilo kutokana na changamoto zinazowakabili wakulima wadogo.

Alisema changamoto kubwa ambayo wakulima wamekuwa wakiipata ni changamoto ya hali ya hewa kama kukosa mvua za kutosha, mafuliko na ukame.

“Kwa kuona hili tumeona kushirikiana na Serikali na wadau wengine ili kumkwamua mkulima kutoka katika majanga mbalimbali, kupitia bima ya kilimo ambapo inajumuisha mazao na mifugo” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Elirehema Doriye alisema NIC kwa kuona umuhimu mpango huo watashirikiana na wadau mbalimbali pamoja na kutoa vipaumbele maagizo ya Serikali.

“Katika hatua ambazo tulizifanya ni kushirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, wakiongozwa na IFAD ambao wamekuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo ya kilmo Tanzania” alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz