Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TIC yaweka rekodi mpya uzalishaji

TIC UWEKEZAJI (600 X 435) TIC yaweka rekodi mpya uzalishaji

Fri, 22 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili miradi mipya 476 ambayo ni ongezeko la asilimia 26 ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo kilisajili miradi 285 yenye thamani ya shilingi bilioni 4.6.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TIC, Binilith Mahenge mkoani Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji wa kituo hicho kwa kipindi cha Januari hadi Novemba 2023 ambapo amesema wanatarajia kusajili miradi 500 hadi ifikapo Desemba 31 mwaka huu.

Ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Tatu wa TIC, uandaaji wa mpango mkakati mpya wa miaka mitano (2023/24-2027/28) umekamilika na kwamba utavutia wawekezaji zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live