Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TIC yasajili miradi ya uwekezaji 227 ya Sh4 trilioni

TIC yasajili miradi ya uwekezaji 227 ya Sh4 trilioni

Tue, 29 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Taifa cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Geofrey Mwambe  amesema kwa kipindi cha miezi 9 ya mwaka huu, imeandikisha uwekezaji wa miradi 227 yenye thamani ya zaidi ya Dola bilioni 2 (Sh4 trilioni).

Akiongea na waandishi wa habari leo Jumatatu, Oktoba 28, 2019, Mwambe amesema miradi hiyo ambayo mingi ni ya sekta ya uzalishaji (viwanda) inatarajia kutoa ajira kwa watu 38,836.

“Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam ndiyo yenye miradi mingi iliyoandikishwa, wawekezaji wengi wapo katika sekta ya uzalishaji, usafirishaji na huduma,” amesema Mwambe.

Amesema sekta ya uzalishaji imeandikisha miradi 128 ikifuatiwa na sekta ya usafirishaji miradi 29, huduma, 18, kilimo 15, utalii 14, majengo 10, rasilimali watu 6, nishati 2, huduma za simu 2 na mali asili 1.

Aidha, Mwambe amesema juhudi za Serikali zinazoendelea katika uboreshaji wa mazingira na kujenga miundombinu ya usafirishaji na uzalishaji wa nishati, utavutia zaidi uwekezaji hapa nchini kwa siku zijazo.

Chanzo: mwananchi.co.tz