Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TIC yasajili miradi 266 mwaka mmoja

85524947e0f9e8f1f14f113c3875f7a9 Kijaji akishuhudia makubaliano

Mon, 28 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), kimeweza kusajili miradi 266 katika kipindi cha mwaka mmoja, ikiwa ni usajili wa miradi ya uwekezaji mingi kwa kipindi kifupi cha mwaka mmoja.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Dk. Ashatu Kijaji, wakati wa hafla ya kukabidhi kiwanja namba 1 kitalu B, eneo la Kwala Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, kwa mwekezaji wa Kampuni ya Sino Tan (Kibaha Industrial Park Ltd), kwa ajili ya Kongani ya viwanda.

Kijaji amesema kuwa wingi wa miradi hiyo, haijawahi kusajiliwa kwa muda mfupi ndani ya mwaka mmoja tangu nchi imepata uhuru, lakini uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, umefanya ndani ya mwaka mmoja.

Amesema mradi huo wa wawekezaji kutoka China ni ushuhuda wa mkakati wa Taifa wa ajenda ya viwanda kufikia pato la kati ifikapo mwaka 2025.

"Manufaa ya uwekezaji huu ni uhakika wa soko la malighafi, ambapo mikataba iliyosainiwa ni ya viwanda vya kuchakata mazao, ambapo Watanzania wanaenda kunufaika na soko, kwani kwa sasa liko hapa tuanze nyumbani tutambue umuhimu wa mradi hata kujifunza Kichina.

“Madiwani wawape elimu wakinamama na watoto juu ya umuhimu wa kutumia eneo hilo la uwekezaji la Kwala," alisema Kijaji.

Alisema mradi huo ni mkubwa Kusini mwa Afrika na Jangwa la Sahara na nchi inatekeleza kauli ya Rais kuwa Tanzania inakuwa nyumbani kwa wawekezaji, ambapo alisisitiza umuhimu wa kuweka mazingira wezeshi kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kwa maslahi ya nchi

"Ujenzi wa Kongani kama hii ni miradi inayoendelea kusajiliwa katika kituo cha uwekezaji na viongozi wa CCM mlisema tuajiri ajira milioni nane ndani ya miaka mitano, inaweza kutengeneza zaidi ya hizo, wito kwa wawekezaji ndani na nje waje kuwekeza na manufaa kwa pande mbili wao na sisi.

“Tanzania ni sehemu salama ya kuwekeza mitaji yao, uwekezaji na biashara hustawi kujituma kuaminiana na uhusiano wa muda mrefu," alisema Kijaji.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara, alisema upatikanaji wa ardhi ni jambo kubwa kuliko kitu chochote, ndiyo maana sheria zinabadilishwa ardhi ipatikane haraka, ili mradi ufanyike kwa haraka.

Kwa upande wake mwakilishi wa Sino Tan Kibaha, Jensen Huang alisema mradi huo umegharimu dola za Marekani 150, ikiwa ni gharama za upatikanaji ardhi, miundombinu na vifaa na utatoa ajira 100,000 za moja kwa moja.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge, alisema kuwa wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwani anafanya jitihada kuweka mazingira bora ya uwekezaji nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live