Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeingia makubaliano ya ushirikiano na Benki ya Azania kwa lengo mahsusi kutanua wigo na kuongeza uzoefu kwenye masuala mbalimbali kupitia ushirikiano na Taasisi nyingine.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Ofisi za TIC jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bw. Gilead Teri amesema wameingia makubaliano hayo na Benki ya Azania ili kutanua wigo na kufika mbali zaidi kwenye uwekezaji.
Makubaliano hayo yanalenga Ushirikiano baina ya Taasisis hizo katika kuboresha na kuongeza ufanisi wa huduma kwa wawekezaji nchini hususan Wawekezaji wa Ndani, Kati ya Maeneo Muhimu ya Ushirikiano ni pamoja na Benki ya Azania Kukisaidia Kituo cha Uwekezaji kukamilisha Mfumo wa Unganishi wa Kielektroniki “Tanzania Electronic Intergrated Investment Window” kwa lengo la kuleta ufanisi na tija katika kuwahudumia Wawekezaji kupitia Kituo cha Huduma kwa Wawekezaji Mahala Pamoja “One Stop Facilitation Centre”.
Teri ameishukuru Menejimenti ya TIC kuwa tayari kushirikiana na Benki ya Azania ni kufanya kazi pamoja ili kuboresha huduma kwa ajili ya Wawekezaji wa ndani na nje nchi .
“Wateja wa Benki ya Azania watahudumiwa na TIC huku kazi ya benki wao Benki hiyo watasaidia kuboresha mifumo zaidi kwenye Kituo chetu cha utoaji wa huduma za pamoja (One Stop Facilitation Centre), ameeleza
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Sheria wa Benki ya Azania, Charles Mugila amesema wamefurahi kufika makubaliano ya ushirikiano na TIC kwa lengo mahsusi la kufanikisha uwekezaji nchini Tanzania.
“Tunaamini ushirikiano huu, Uwekezaji nchini utafika mbali na hatimaye kukuza Uchumi wetu wa nchi kupata maendeleo zaidi ikiwa pamoja na kutoa fursa za ajira nyingi nchini,” amesema Mugila.