Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFS yakabidhi mizinga ya nyuki 100 Msomera

NYUKI MMMK TFS yakabidhi mizinga ya nyuki 100 Msomera

Wed, 31 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wamekabishi mizinga 100 ya kufugia nyuki yenye thamani ya Sh milioni 10 kwa vikundi vitatu vilivyopo kwenye Kijiji cha Msomera wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. - Akikabidhi mizingi hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba,Kamanda uhifadhi Kanda ya Kaskazini, James Nshare amesema kuwa lengo la kutoa mizinga hiyo ni kwa ajili ya njia mbadala ya kuwaongezea kipato na kulinda misitu. - "Kupitia mizinga hii wananchi wataweza kufanya shughuli za ufugaji lakini na kulinda misitu yetu isiweze kuharibiwa kwa moto sambamba na kuchunga ndani ya misitu"amesema Nshare. - Hata hivyo Mkuu wa mkoa, Waziri Kindamba amesisitiza utunzaji wa mazingira na kuacha tabia za kukata miti hovyo ili kujilinda na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wamekabishi mizinga 100 ya kufugia nyuki yenye thamani ya Sh milioni 10 kwa vikundi vitatu vilivyopo kwenye Kijiji cha Msomera wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. - Akikabidhi mizingi hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba,Kamanda uhifadhi Kanda ya Kaskazini, James Nshare amesema kuwa lengo la kutoa mizinga hiyo ni kwa ajili ya njia mbadala ya kuwaongezea kipato na kulinda misitu. - "Kupitia mizinga hii wananchi wataweza kufanya shughuli za ufugaji lakini na kulinda misitu yetu isiweze kuharibiwa kwa moto sambamba na kuchunga ndani ya misitu"amesema Nshare. - Hata hivyo Mkuu wa mkoa, Waziri Kindamba amesisitiza utunzaji wa mazingira na kuacha tabia za kukata miti hovyo ili kujilinda na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi. "Tunataka Kijiji hiki cha Msomera kiwe cha mfano katika utunzaji na uhifadhi wa misitu kwenye eneo hili kwa kulinda misitu hiyo na kutofanya uharibifu"amesema RC Kindamba -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live