Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFS yaja kivingine ufugaji wa nyuki

Bc674d4d6fe36f30510eafbc1baa5c33 TFS yaja kivingine ufugaji wa nyuki

Fri, 15 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS), Wilaya ya Geita imedhamiria kuimarisha uwekezaji wa sekta ya ufugaji wa nyuki kwenye maeneo ya hifadhi, ambapo imelenga kuvuna kilo 1000 za asali kwa mwaka ujao wa fedha.

Hayo yameelezwa na Ofisa Mhifadhi wa TFS, Wilaya ya Geita, Almas Mggalu, wakati akizungumuza na waandishi wa habari, baada ya kutembelea maeneo ya hifadhi ya msitu Geita.

Mggalu amesema, TFS Geita walianza ufugaji wa nyuki, mwaka jana wakiwa na mizinga 24 na kuvuna takribani kilo 50 za asali na sasa wamenunua mizinga 100 na kufikisha jumla ya mizinga 124 kwenye manzuki tatu tofauti.

“Lakini tunatarajia kuwa na uvunaji mkubwa kwa sababu tumepanua uwigo kwa kuongeza mizinga kwa kutafuta maeneo mengine, ambayo ni muhimu kwa ajili ya ufugaji nyuki,” amesema.

“Kwa hiyo sasa hivi kitu ambacho kinaendelea tunakamata yale makundi ya nyuki, na kuna mizinga tayari nyuki wameingia, sasa tunaendelea kukagua kwa nini baadhi ya nyuki hawajaingia,” amesema.

Amesema wamejipanga kutoa elimu zaidi kwa wananchi, ili wahamasike kufanya ufugaji wa nyuki na uvunaji wa kisasa wa asali, ili kuchagiza hatua ya uhifadhi wa misitu kupitia shughuli hiyo mbadala ya kiuchumi.

Mggalu amesema hadi sasa TFS imetoa ruhusa kwa wananchi kufuga nyuki bure katika eneo la hifadhi ya msitu wa Geita na tayari wameshaanza kujitokeza na wanafuga kwa kufuata muongozo na usimamizi wa TFS.

“ Kikubwa ni wao tu wanakuja wanaleta maombi ofisini kwetu, tunawapa kibali na kuwaonesha kwamba eneo gani wataweka mizinga yao na tunakaribia mizinga 800 ambayo hii ni ya wanazengo,” amesema.

Mkuu wa wilaya ya Geita, Wilson Shimo, amesema wanaunga mkono juhudi za TFS kwa kuhamasisha upandaji miti na kudhibiti shughuli za uharibifu wa mazingira, ili kukuza sekta ya ufugaji wa nyuki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live