Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFS yaita wadau kuwekeza katika utalii wa ikolojia

MSITU Kilosa TFS yaita wadau kuwekeza katika utalii wa ikolojia

Mon, 5 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika kuhakikisha fursa za uwekezaji katika sekta ya misitu nchini inaongezeka, Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) imetoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza kwenye maeneo yaliyotengwa ndani ya misitu hiyo kwa ajili ya shughuli za utali ikolojia.

Akizungumza leo Jumapili Juni 4, 2023 katika maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya Karibu Kilifair yanayoendelea katika Viwanja vya Magereza jijini hapa, Mkuu wa sehemu ya kutangaza utalii ikolojia kutoka TFS, Anna Lauo amesema fursa za uwekezaji zipo. Amesema kwa sasa utalii ikolojia unaofanywa ndani ya misitu unakua kwa kasi kubwa hivyo ni fursa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika maeneo hayo kwa kujenga hoteli zisizoharibu mazingira.

"Kwa sasa wageni wengi wanakuja ila wanakosa huduma za malazi na vyakula hivyo tunahamasisha wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika hiyo misitu walete maombi ya kujenga hoteli zisizoharibu mazingira, kwa mfano kwenye shamba letu la misitu Sao Hill kumekuwa kukifanyika mashindano ya magari ila wanakosa pa kulala,"amesema Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Zara Tours, Zainab Ansell amehimiza Watanzania kuendelea kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo hapa nchini ikiwemo kupanda Mlima Kilimanjaro pamoja na utalii wa asili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live