Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TCRA kuwatumiaji ‘magwiji mitandaoni’ kuhamasisha usajili wa laini za simu

87289 TCRAPIC TCRA kuwatumiaji ‘magwiji mitandaoni’ kuhamasisha usajili wa laini za simu

Fri, 6 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ili kusajili watu wengi zaidi kwa alama za vidole kabla ya siku ya mwisho, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepanga kuwashirikisha watumiaji maarufu wa mitandao ya kijamii kufanikisha lengo hilo.

Serikali ilitangaza kwamba Desemba 31 kila mtumiaji wa simu ya mkononi anatakiwa kuwa amekamilisha mpango huo lakini zikiwa zimebaki siku chache waliotekeleza ni wachache.

Mwaliko uliotolewa Novemba 29 na kaimu mkurugenzi mkuu wa TCRA, Dk Emmanuel Manasseh unawakaribisha watumiaji mashuhuri wa mitandao ya kijamii hasa Instagram, Twitter, Facebook na Youtube kwenye warsha itakayofanyika kesho katika Hoteli ya Serena kuanzia saa 3:00 asubuhi.

“Lengo la warsha hiyo ni kutoa elimu kuhusu usajili wa laini za simu kwa njia ya biometria na umuhimu wake kwa watumiaji wote wa mitandao ya kijamii nchini,” amesema Dk Manasseh.

Licha ya watuamiaji hao wenye wafuasi wengi zaidi mtandaoni, TCRA imewakaribisha waandishi wa habari kushiriki warsha hiyo.

Meneja mawasiliano wa mamlaka hiyo, Semu Mwakianjala amesema mpaka Novemba 30 watumiaji milioni 18 walikuwa wamejiandikisha hivyo uhamasishaji unaendelea kufanywa kuwashawishi wengi zaidi kujitokeza.

Usajili wa laini hizo unahitaji kitambulisho cha Taifa ambavyo wananchi wengi hawana mpaka sasa ingawa jitihada za kuvitoa zinaongezwa. Takwimu za TCRA zinaonyesha kuna zaidi ya laini milioni 43 zilizosajiliwa kikawaida.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz