Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TCRA inavyoupigia rada uchumi wa buluu

OchQ8Gi5.jpeg TCRA inavyoupigia rada uchumi wa buluu

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imezitaka shule na vyuo vikuu nchini, kuanzisha klabu za kidijitali zitakazowawezesha wanafunzi wao kujifunza juu ya masuala yanayohusu teknolojia za kidigitali katika uchumi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo ofisi ya Zanzibar na kusambazwa kwa vyombo vya habari jana Novemba 13, Meneja wa TCRA Zanzibar, Esuvatie Masinga amesema uanzishwaji wa klabu hizo, utachochea hamasa ya wanafunzi kujifunza zaidi.

“Hizi klabu zitachangia kuchochea hamasa ya wanafunzi kujifunza masuala ya teknolojia za kidijitali, ambayo ni muhimu katika zama hizi ambapo uchumi wa nchi na dunia unategemea sana teknolojia,” amesema na kuongeza;

"Tunawahimiza wanafunzi wa ngazi zote kujiunga na klabu za kidijitali au kuanzisha klabu hizi kwenye taasisi zao ambazo zitakuwa na nafasi ya pekee katika kuhamasisha kujifunza masomo ya STEM (Sayansi, Teknolojia, Uhandisi, na Hisabati) na kuwa washiriki wenye mchango chanya katika uchumi wa buluu na kidigitali.”

Kwa mujibu wa Meneja huyoi, taasisi za elimu zinazopenda kuanzisha vilabu vya kidijitali vya wanafunzi zinapaswa kuwasiliana na TCRA na hivyo kuelekezwa namna ya kufanya ili klabu hizo ziweze kuwa na tija kwa kwa wanafunzi na nchi kwa ujumla.

Kwa upande mwingine TCRA Zanzibar imewataka waombaji wa leseni za mawasiliano kutumia mfumo wa kieletroniki ujulikanao kama ‘Tanzanite Portal’ katika kuwasilisha maombi yao, huku ikiwataka wananchi kutumia huduma za mawasiliano zilizosajiliwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, TCRA Zanzibar imeanzisha kampeni kupitia vyombo vya habari, lengo likiwa ni kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kutumia huduma za mawasiliano zilizosajiliwa.

Akizungumza katika mahojiano na vituo vya redio vya Mkoani na Micheweni, Masinga, amesisitiza azma ya mamlaka, ya kukuza sekta ya mawasiliano kwa kuzingatia usalama wa watumiaji.

"Tunawaomba wananchi watambue umuhimu wa kutumia huduma za mawasiliano zilizosajiliwa, hasa wale wanaosafirisha vifurushi na vipeto, wahakikishe wanaowasafirishia wana leseni ya TCRA," amesisitiza.

Mamlaka hiyo, inayosimamia sekta ya mawasiliano nchini, imebainisha kuwa watumiaji wa huduma za mawasiliano zilizosajiliwa wanajilinda zaidi na wanaweza kufuatilia haki zao kwa urahisi wanapotumia huduma hizo.

Aidha, mfumo huo unawezesha mamlaka kuwasiliana moja kwa moja na watoa huduma na kuwapa usaidizi kuhusu shughuli zao za mawasiliano, ikiwa ni pamoja na simu, intaneti, utangazaji, na huduma za kiposta kama vile usafirishaji wa vifurushi na vipeto. Mwisho

Chanzo: www.tanzaniaweb.live