Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TCDC yaja na mkakati kukuza biashara

Digitalllll TPDC yaja na mkakati kukuza biashara

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamisheni ya Maendeleo ya Ushirika nchini (TCDC) imeanza kutekeleza mpango wa kubadili namna ya kuendesha vyama vya ushirika na kuviwezesha kutumia teknolojia za kisasa katika kufanya shughuli zao.

Mwenyekiti wa TCDC Abdulmajid Nsekela ametoa taarifa hiyo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa ushirika uliokuwa na lengo la kujadili maendeleo ya ushirika na kuweka mkakati wa kuimarisha sekta hiyo nchini.

Nsekela amesema uwekezaji katika mifumo ya kisasa ya kidijitali itaongeza ufanisi wa kiutendaji katika vyama vya Ushirika pamoja na mamlaka za usimamizi wa sekta hiyo.

Kwa upande wake Mrajisi wa Ushirika nchini Dkt. Benson Ndiege amesema, lengo la mkutano huo wa wadau wa ushirika ni kujadili maendeleo ya ushirika na kuweka mkakati wa kuimarisha sekta hiyo hapa nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live