Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TCB kunoa vikundi vya wanawake kiuchumi

839f525ab461a16f9dd9caa1e27724b6 Benki ya TCB yaahidi neema Kagera

Sat, 2 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Biashara nchini (TCB), imeahidi kuongeza ubunifu na kutoa huduma zaidi kwa vikundi vya wanawake wanaotaka kujikwamua kiuchumi.

Akifungua tawi la TCB mkoani Kagera, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, alisema wanawake wamekuwa mstari wa mbele kujiunga na huduma za taasisi za kifedha, huku asilimia kubwa ya wanawake wanaochukua mikopo kujikwamua kiuchumi wakirejesha fedha kwa uaminifu mkubwa.

Alisema ili kuendelea kutambua mchango mkubwa wa wanawake, benki hiyo inajipanga kuimarisha vifurushi vya kuwawezesha hata wanawake wajasiriamali wadogo na wanawake wa chini kabisa kupata huduma.

" Benki hii ni muunganiko wa benki nne, ikiwemo benki ya yawanawake katika tathimini zetu tumeona wanawake wengi ni waaminifu sana, wanarejesha wana bidii katika kutafuta na kujiinua kiuchumi,” alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mosses Machali, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Charles Mbuge aliomba benki hiyo kufikiria kupunguza, riba ili kupata wateja wengi zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live