Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TCAA yatoa pole ajali ya Ethiopia Airline

46137 Pic+tcca TCAA yatoa pole ajali ya Ethiopia Airline

Mon, 11 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetuma salamu za rambirambi kufuatia ajali ya ndege ya Shirika la Ethiopia Airlines iliyoanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, Addis Ababa, Ethiopia kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), Nairobi Kenya.

Taarifa iliyotolewa jana Jumapili Machi 10, 2019 na mkurugenzi mkuu wa TCAA, Hamza Johari imeeleza kuwa mamlaka hiyo imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya ndege hiyo namba za usajili ET 302 iliyopoteza mawasiliano na kituo cha kuongoza ndege cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga Ethiopia, dakika sita baada ya kuruka.

“Salamu za rambirambi ziende kwa familia za abiria na wafanyakazi wa ndege waliopoteza maisha. Ajali hii ya kusikitisha imeathiri jumuiya yote ya wana usafiri wa anga duniani. Tunasubiri majibu ya kiuchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Katika ajali hiyo, watu wote 157 waliokuwamo wamepoteza maisha.



Chanzo: mwananchi.co.tz