Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBS yawanoa wakulima wa alizeti

Wakulima Alzeti TBS yawanoa wakulima wa alizeti

Tue, 19 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

Wakulima na wasindikaji wa mafuta ya alzeti mkoani Katavi wamepewa mafunzo ambayo yatawasaidia kuongeza upatikanaji wa mafuta bora yatakayouzika ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mafunzo hayo yalioanza jana na kumalizika leo oktoba 19, 2021 Kaimu Meneja Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kanda ya Magharibi Rodney Alananga, amesema moja ya lengo la mafunzo hayo ni kutimiza azima ya serikali ya kuboresha mfumo wa mafuta nchini.

Amesema mafuta ambayo yanazalishwa yanatakiwa yakidhi viwango vya kitaifa na kimataifa pia wajue ni vifungashio gani vinatakiwa katika kufungasha mafuta hayo pamoja na viwango vya mafuta ambayo yanatakiwa kutumika.

"Tunataka tuone mafuta ambayo wameya chakata yamewekwa rebo au alama ya ubora yanayotoka katavi yakiuzwa kwenye supa maketi mbalimbali na badaye tuyaone nchi jirani kama vile zambia, congo na kwingineko," amesema Alananga.

Afisa mdhibiti ubora wa shirika hilo, Gudula Boniface, amewataka wakulima na wasindikaji hao wazingatie viwango na kanuni bora ambazo amewaelekeza ili waweze kufikia lengo lililokusudiwa ikiwemo kujenga majengo ya kusikia mafuta yasiyopitisha mdudu wa ainayeyote.

Amesema endapo kila kitu kikifanyika kwa ubora kuanzia kulima hadi kubadilisha malighafi kuwa bidhaa kutazuia upotevu wa malighafi na kuzuia uharibifu wa muda mfupi.

Afisa mazao wa Manispaa ya Mpanda, Gastor Mwakilembe, amesema mkulima inatakiwa aandae shamba mapema mwezi mmoja kabla ya kilimo cha alizeti na azingatie kuvuna kwa muda sahihi baada ya alizeti kukomaa.

Amesema lengo lao ni kumtoa mkulima kwenye kilimo cha mazoea cha kuvuna gunia nne kwa hekari moja na badala yake waanze kuvuna gunia 18 kwa hekari moja lakini pia waepuke kurudia mbegu wakati wa kupanda.

"Wakati wa kupanda lazima achague mbengu atumie izi mbegu za kisasa na azingatie taratibu zote tulizomfundisha leo hapa kuanzia kundaa shamba, kupalilia, kupanda kwa kuzingatia vipimo sahihi na kupalia ni kuanzia wiki mbili za mwanzo, kuweka mbolea ya kupandia," amesema.

Amesema udongo unaotakiwa kwa kilimo cha alizeti ni tifutifu wenye rutuba na wenye kuhifadhi unyevunyevu hivyo amewataka wasichanganye zao hilo na mazao mengine isipokua zao la mahindi kutokana na mmea huo kukua kwa kuelekea juu kama ilivyo alizeti.

Afisa maendeleo ya jamii, Anna Shumbi, ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, amesema azima ya serikali ni kuhakikisha nchi yetu inajitosheleza katika uzalishaji wa mafuta ya kula ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha kwa kuagiza mafuta kutoka nje.

Amesema takwimu za karibuni zinaonyesha mahitaji ya mafuta ya kula kwa mwaka ni takribani tani lakitano na sabini ikilinganishwa na uzalishaji wa ndani ambao ni tani lakimbili na tano hivyo kuna upungufu wa tani lakitatu na stini na tano.

Meneja wa kiwanda cha kusindika na kukamua mafuta cha Nondo Investors Campany Limited, Fakili Alikaniki, ni mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo amesema upatikanaji wa malighafi bado ni tatizo hivyo ameiyomba serikali kuendelea kuhamasisha kilimo cha alizeti.

Hata hivyo, amesema wao kama wawekezaji wanaposafirisha mazao kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine wakifika njiani wanazuiwa hasa katika mkoa wa Tabora na kusababisha bidhaa kuharibika kwa kukaa muda mrefu kwa kigezo cha kukosa leseni ya kununua kuuza na kusafirisha.

Ameiomba serikali kuangalia suala hilo na kama hizo, leseni zipo basi zitolewe ili kuepusha huo usumbufu kwani wamejaribu kufuatilia ofisi husika wameambiwa leseni hizo, hazipo hivyo wamepewa leseni ya kuuza na kununua ambayo haiwasaidii wanaposafirisha mazao yao.

Chanzo: ippmedia.com