Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBS yawafunda wafanyabiashara mazao ya chakula

Wafanyabiashara Pic Data TBS yawafunda wafanyabiashara mazao ya chakula

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Habari njema kwa wafanyabiashara wa mazao ya chakula nje ya nchi baada ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kufungua milango ya utoaji semina ya utambuzi wa viwango vinavyohitajika katika masoko ya nje.

Kwa mujibu wa TBS, kipaumbele cha Serikali katika mafunzo hayo kwa sasa ni kundi la wafanyabiashara wapya wa mazao ya chakula ikiwamo mahindi. 

Aidha, TBS imesema huduma hiyo itaendelea kutolewa kulingana na mahitaji ya wakati husika.

Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa miezi 11 imepita baada ya Mamlaka ya Ushuru nchini Kenya kusimamisha uingizaji wa mahindi kutoka Tanzania na Uganda kwa madai ya kuwa na sumu ya Mycotoxin.

Tukio hilo liliporomosha thamani ya uuzaji wa mahindi nchini humo kwa asilimia 73 kama ilivyoelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Peter Manya nchini humo huku mamia ya wafanyabiashara wakikabiliwa na changamoto ya uhaba wa masoko ya nje.

Akizungumza leo Februari 17,2022 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo, David  Ndibalema amesema umuhimu wa mafunzo hayo ni kutambua mahitaji ya soko ili kuepuka usumbufu wa nchi unayopeleka bidhaa hizo.

Advertisement David amesema katika hatua za uhakiki, TBS itachukua sampuli ya bidhaa ya mfanyabiashara na kuipima maabara kabla ya kupatiwa cheti.

“Hicho cheti kitamsaidia kuuza mazao yake huko nje, sasa mafunzo hayo ni hiyari tunashauri wajitokeze kujifunza na kuthibitishwa bidhaa zao kabla ya kusaifirisha. Cheti kitatolewa kwa kila mzigo unaposafirishwa,”amesema David.

David amesema cheti hicho kinatambuliwa na katika masoko ya nchi husika wanazopeleka ikiwamo Afrika Mashariki chini ya makubaliano ya sheria inayoweka viwango vya pamoja.

Hussein Ahmed Ally, mmliki wa Kampuni ya Novoten inayotaka kuanza kusafirisha mihogo na matunda ya pasheni nchini Irani amesema mafunzo hayo yatasaidia tishio la kupata hasara.

“Tanzania tunazalisha mihogo karibu aina 10 zenye viwango tofauti vya ubora sasa huwezi kujua nchi gani wanahitaji viwango gani, usipojua unaweza kupeleka ukapata hasara,”amesema Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live