Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBS yawafikia wadau wa sekta ya utalii

WILAYA 1080x640.jpeg Said Mtanda akifungua mkutano huo

Wed, 30 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miongoni mwa sababu zinazozifanya bidhaa na huduma za nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kushindwa kupenya na kuingia katika masoko ya kimataifa ni kushindwa kwa bidhaa na huduma hizo kukidhi matakwa ya viwango jambo ambalo linaweza kuwakosesha uwanda mpana wa biashara kimataifa.

Akizungumza katika ufunguzi wa warsha ilioandaliwa na shirika la Viwango Tanzania TBS na kuudhuriwa na wadau wa sekta ya utalii kanda ya kaskazini mkuu wa Wilaya ya Arusha Said Mtanda amesema kuwa kupitia warsha hiyo watakwenda kufaidika kwa kuelimishwa kuhusu viwango katika sekta ya utalii vinavyotolewa nchini.

Amesema kuwa kwa wadau kufahamu viwango katika sekta ya utalii kutaongeza thamani kwenye maeneo mbalimbali ya huduma za utalii lakini pia kuendelea kujenga na kukuza taswira ya nchi yenye vivutio vyenye ubora duniani.

Amesema wakati mwingine bidhaa na huduma hushindwa kuingia katika soko la kimataifa au la kikanda kutokana na utofauti katika matakwa ya kiwango cha bidhaa na huduma husika baina ya nchi na nchi.

“iwapo itakuwa na uwianishaji wa matakwa katika viwango baina ya nchi na nchi na hatimaye kuwa na viwango sawa kikanda na kimataifa kutawezesha uwanja wa biashara kimataifa kuwa sawia”. Amesema DC Mtanda.

Aidha DC Mtanda ameipongeza TBS kuendelea kutoa elimu ya viwango kwa wadau mbalimbali kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa na kuingia nchini ziinakidhi viwango vinavyotakiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live