Dar es Salaam. Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limetangaza viwango vinavyotakiwa kwa wazalisha, wasambazaji na waingizaji wa mifuko ya aina ya non-woven (kitambaa chepesi) inayotumika kubebea bidhaa mbalimbali.
Viwango hivyo vimetangazwa jana Ijumaa Juni 21, 2019 na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk Athuman Ngenya wakati akizungumza na wanahabari Dar es Salaam.
Dk Ngenya alisema mifuko kwa sasa lazima izingatie matakwa ya msingi ambayo ni uzito usiopungua gramu 70, iwe yenye kuweza kurejelezwa, iwe na anuani ya mzalishaji au nembo ya biashara, ioneshe uwezo wa kubeba na iwe imethibitishwa na TBS.
“Hakuna mfuko wowote utakaoruhusiwa kuingia au kuzalisha nchini kama hautakidhi matakwa yaliyotajwa. Tunatoa onyo kwa watakaoendelea kusambaza, kuzalisha au kuingiza mfuko uliopo kinyume na utaratibu ulioanishwa na hatua za kali zitachukuliwa dhidi yao,” alisema Dk Ngenya.
Aprili 9 mwaka 2019, Serikali ya Tanzania ilitangaza kupiga marufuku matumizi ya mfuko plastiki ifikapo Juni Mosi, agizo ambalo limeanza kutekelezwa.
Akizungumzia hatua hiyo, mwakilishi wa wazalishaji na watengenezaji wa mifuko mbadala, Allen Kimambo alisema hatua nzuri kwa TBS kuweka viwango ambavyo vitasaidia kukuza sekta ya mifuko ya karatasi inayotumika kama mbadala sasa.
Pia Soma
- Spika wa Bunge la Georgia ajiuzulu
- Kaka asimulia alivyonusurika ajalini, ilivyoua bibi harusi na wenzake
- Asali, mdalasini hutibu magonjwa lukuki