Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBS yatoa msimamo huu ukaguzi wa magari

De3fee4719938666113e593e75e980e6 TBS yatoa msimamo huu ukaguzi wa magari

Wed, 20 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema kuanzia Leo Julai 20,2022 magari yote yaliyotumika yanayotoka nchini Japan yatakuwa yanakaguliwa nchini humo kabla ya kuja Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Saalm, Meneja wa Usimamizi wa shehena zinazoingia na kutoka nchini, Mhandisi Mohamed Mkwawa amesema lengo ni kupunguza muda wa ukaguzi.

"Sasa gari linakuja na cheti cha ubora linaenda kwenye kaguzi zingine faida yake wakati mwingine magari yanakuja yakiwa na mapungufu, hivyo sasa inakaguliwa huku huko hivyo yanayoingia ni yenye ubora,"amesema.

Mkwawa ameeleza kuwa ukaguzi wa magari hayo nchini Japan utafanywa na Kampuni iitwatayo EAA Company

Limited ya nchini humo na gharama ya ukaguzi utakaofanyika ni dola za kimarekani 150 kwa gari, hivyo hakuna ongezeko lolote la gharama za ukaguzi.

"Magari ambayo tayari yalikuwa yameshanunuliwa na yako kwenye mchakato wa kusafirishwa au yalishapakiwa kwenye meli kwa ajili ya kusafirishwa kuja hapa nchini kabla ya tarehe 20 Julai 2022, yatakaguliwa na TBS yatakapofika nchini bila adhabu yoyote,"amesisitiza.

Amesema utaratibu wa kukagua magari kabla ya kuwasili nchini (Pre-Shipment Verification on Conformity to Standards (PVoC) utasaidia kuepuka gharama za matengezo kwa wanunuaji wa magari.

Mkwawa amebainisha kuwa Shirika linaendelea na taratibu za kupata mawakala kwa ajili ya ukaguzi wa magari yanayotoka nchi za Uingereza, Dubai na Singapore.

" Utaratibu wa nchi hizo utakapokamilika basi waingizaji na wafanyabiashara wa magari watapewa taarifa,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live