Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBS yateketeza katoni 60 za nyaya feki

Da01d0b808d4a54213b7bc81f1875edd TBS yateketeza katoni 60 za nyaya feki

Sun, 29 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) kupitia ofisi yake ya Kanda ya Ziwa imeteketeza shehena ya katoni 60 zenye pisi zaidi ya nyaya 7,000 za kusambaza umeme wa majumbani.

Akizungumza wakati wa uchomaji wa nyaya hizo feki, Ofisa Mdhibiti Ubora kutoka TBS, Arnold Kubingwa alisema nyaya hizo walizoteketeza zina gharama ya zaidi ya Sh milioni tano.

Kubingwa alisema bidhaa hizo ziliingizwa nchini kinyemela na baada ya kupimwa zilikutwa hazikidhi na hivyo kuteketezwa ili zisiingie sokoni na kuleta madhara kwa watumiaji.

Alisema walipima nyaya hizo za umeme na kugundua zinaingiza umeme mkubwa sana jambo linaloweza kusababisha shoti kubwa katika nyumba.

Aliwaomba wateja kuhakikisha wanaangalia taarifa za bidhaa endapo kama bidhaa hizo zitakuwa na kasoro ni vyema wakahakikisha wanaziripoti kwa shirika lao.

Kubindwa alisema shirika lao litaendelea kusimama na kuhakikisha kuwa bidhaa zote zinakidhi matakwa ya viwango husika kabla ya kusafirishwa na kuingia nchini.

Aliwataka wadau wa usafirishaji na wafanyabiashara kuhakikisha wanaagiza bidhaa zenye ubora nje ya nchi.

Alisema TBS itaendelea kulinda jamii kutokana na bidhaa hafifu ambazo zinahatarisha afya, usalama na mazingira.

Mkazi wa Buhongwa Baraka Usaka, aliliomba hilo la TBS kuhakikisha linadhibiti bidhaa zote feki zisifike kwa wananchi ili kuepusha watu kupata madhara ya kiafya au majanga ya moto yanayotokana na umeme.

Chanzo: habarileo.co.tz