Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBS yapata cheti cha kimataifa cha ithibati ya mifumo

Tbs Pic.jpeg Sehemu ya menejimenti ya TBS

Fri, 13 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Viwango Tanzania (TBS),limepokea cheti cha kimataifa cha ithibati cha utoaji huduma uthibitishaji wa mifumo ya kimenejimenti huku Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara,Exaud Kigahe ameipongeza TBS kwa hatua hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea cheti hicho kutoka Huduma za Ithibati za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADCAS) leo Mei 12,2022 Jijini Dodoma,Naibu Waziri Kigahe amesema huo ni uthibitisho na ushuhuda tosha kuwa TBS inaendelea kujizatiti na kutambulika kimataifa kupitia utekelezaji wa majukumu yake.

Kigahe amesema kuwa ithibati ina manufaa makubwa kwa taasisi za umma na binafsi na TBS inatoa huduma kwa gharama nafuu ikilinganishwa na gharama zinazotozwa na kampuni za nje ambazo zimekuwa zikitoa huduma hizo.

“Niwapongeze TBS kwa kufikia hatua hii kubwa ya kupata ithibati ya umahiri katika kutoa huduma ya ithibati ya umahiri katika kutoa huduma hii, sina shaka mtaendelea kudumisha na kuongeza wigo kwenye kutoa huduma zenye ithibati ya umahiri ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa taifa,”amesema Mhe.Kigahe

Aidha amesema kuwa hivi karibuni,makampuni ya nje yalipata changamoto kutokana na janga la UVIKO-19 hivyo kushindwa kutoa huduma kwa wateja wao,hali iliyopelekea wateja wao kupoteza uhalali wa kuwa na vyeti vya uthibitisho wa mifumo ya kimenejimenti.

''kutokana na tatizo hilo baadhi ya taasisi tayari zimefanya uhamisho wa kupata huduma ya uthibitisho wa mifumo ya kimenejimenti kutoka kampuni za nje kwenda TBS ili kunufaika na huduma ya uhakika kwa gharama nafuu.''amesema

Hata hivyo ametoa wito kwa taasisi za umma na sekta binafsi kuthibitisha mifumo yao ya kimenejimenti kwa kuitumia TBS ambayo imepokea cheti cha Kimataifa cha ithibati katika huduma hii.

''Tutaendelea kuisaidia TBS katika kutimiza majukumu yake na kuhakikisha inaendelea kuwahudumia wananchi kwa umahiri na ufanisi katika nyanja zote za uzalishaji bidhaa na utoaji huduma kwa mujibu wa sheria ya viwango Na.2 ya mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake''amesema Naibu Waziri

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS, Lazaro Msasalaga, ametaja hatua mbalimbali za kupata cheti hicho kuwa ni pamoja na kuweka na kufuata mifumo kulingana na matakwa yaliyoainishwa kwenye kiwango cha kimataifa ISO/IEC 17021.

“Kujipima utendaji kwa mujibu wa kiwango husika pamoja na matakwa ya tume ya ithibati na kuwa na wataalam wenye umahiri na weledi katika dhana nzima ya utoaji huduma,”amesema Bw.Msasalaga

Awali Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa SADCAS,Bw. Victor Mundembe,ameitaka TBS kuhakikisha inazingatia ubora kwenye utoaji huduma hizo ili viwango vya ithibati hiyo visishuke.

Naye Mkurugenzi Mkuu TBS Dkt.Athuman Ngenya amewataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuwatangazia wananchi, taasisi za umma na sekta binafsi kuwa huduma hiyo kwa sasa ipo TBS.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live