Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBS yamwaga mpunga kwa wajasiriamali

FEDHA WEB TBS yamwaga mpunga kwa wajasiriamali

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) imekuwa ikitenga zaidi ya Sh milioni 250 yenye lengo la kuwahudumia wajasiriamali wadogo nchini bila malipo.

Hayo ameyasema Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk Athuman Ngenya wakati akizungumza na wahariri wa habari na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo ikiwa ni maelekezo ya Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu kwa Taasisi zote za Umma kuzungumzia mipango na mikakati yao.

Mkurugenzi huyo ameongezea kwa kusema kuwa kipindi cha miaka mitatu jumla ya leseni za ubora wa bidhaa 2,106 zimetolewa kwa wazalishaji mbalimbali wa bidhaa hapa nchini sawa na asilimia 105.3 ya lengo la kutoa leseni 2,000 kati ya leseni hizo jumla ya leseni 1,051 zilitolewa bure kwa wajasiriamali wadogo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live