Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBS yakamata tani moja na nusu vipodozi hatari

D4c864f11b0aae72d9b6bbeddd6bca7e.png TBS yakamata tani moja na nusu vipodozi hatari

Sun, 19 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limekamata shehena ya zaidi ya tani moja na nusu yenye bidhaa hafi fu, vikiwemo vipodozi hatari kwa afya ya watumiaji.

Akizungumza na gazeti hili baada ya kazi ya kuteketeza bidhaa hizo jijini hapa, Mkaguzi wa TBS, Julius Panga alisema baadhi ya vipodozi vilikuwa na vifungashio vilivyoonesha kuwa vilitengenezwa nchini Ivory Coast, Senegal na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Alisema kazi ya kukamata bidhaa hizo, ilifanyika kati ya mwezi Machi na Aprili mwaka huu katika mikoa sita ya Kanda ya Ziwa ya Mwanza, Kagera, Shinyanga, Mara, Geita na Simiyu.

“Ilikuwa ni mwendelezo wa kazi ya ufuatiliaji na ukamataji wa bidhaa hafifu sokoni. Tulibaini uwepo wa bidhaa hizo nyingi zilizovushwa kutoka nchi za mbali kama Senegal na Ivory Coast,” alisema.

Mkaguzi huyo aliwashukuru wasamaria wema, wanaoendelea kutoa taarifa za siri kwa shirika hilo juu ya uwepo wa bidhaa hafifu sokoni, licha ya ukweli kuwa bidhaa hizo sasa hivi zinapenyezwa kwa usiri mkubwa sana kuliko huko nyuma.

Panga alisema kuendelea kukamatwa kwa vipodozi vilivyopigwa marufuku sokoni, ni ishara ya wazi kuwa zina wateja wengi wasiojali afya zao, ama wanaozitumia bila kujua athari zake kiafya.

Uchunguzi unaonesha bidhaa nyingi hasa vipodozi hafifu, zinapenyezwa nchini na kuhifadhiwa sehemu za siri sana huku zikisafirishwa usiku kwenye masoko lengwa.

Panga alisema wahusika wote wamechukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria, ikiwemo kulipa faini na kulipa gharama za kuharibu bidhaa hizo.

Chanzo: habarileo.co.tz