Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBS yaendesha oparesheni maalum kwa bidhaa za chakula na vipodozi

TBCS.jpeg Maafisa wa TBS wakiendelea na zoezi la ukaguzi wa bidhaa za chakula na vipodozi

Wed, 2 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Viwango Tanzanaia (TBS) Kanda ya Magharibi limewakamata wafanyabiashara 36 kwa makosa ya kuuza bidhaa zilizoisha muda wa matumizi ( expired date) pamoja na kuuza bidhaa ambazo zimeshapigwa marufuku.

Akizungumza katika Operesheni hiyo Kaimu Meneja Kanda ya Magharibi (TBS) Rodney Alananga amesema wamefanya operesheni maalumu katika mkoa wa Katavi kwa bidhaa za Chakula na Vipodozi kwenye maghala, maduka makubwa ya jumla na rejareja, mipakani na bandarini kwa halmashauri nne na kubaini makosa kwa wafanyabiashara hao.

Amesema bidhaa ambazo zimeshikiliwa na shirika hilo zina thamani ya TZS 5,600,550/= hivyo basi TBS inatarajia kufanya uteketezaji wa bidhaa hizo baada ya taratibu zote za kisheria kufuatwa.

"TBS imechukua hatua za awali kwa kuzuia bidhaa zote zilizoonekana kuwa na makosa ambazo utekelezaji na ufuatiliaji wake utaendelea ndani ya Siku 14 kwa mujibu wa seizure notice mpaka 23/3/2022". Amesema Bw. Alananga.

Katika Operesheni hiyo TBS Kanda ya Magharibi imeshirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo ofisi ya RPC,RAS, RSO, TRA, DC na kufanikisha zoezi hilo ambalo lilifanyika kuanzia Februari 21 hadi 27, 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.live