Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBS waridhishwa mwitikio wa matumizi ya bidhaa zenye nembo

434764593dc7c882c57e79658cc7f7d8.png TBS waridhishwa mwitikio wa matumizi ya bidhaa zenye nembo

Mon, 24 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAOFISA wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamefanya ukaguzi katika viwanda vinavyozalisha vifungashio na usajili wa majengo ya bidhaa za vyakula na vipodozi mkoani Mwanza, huku wakielezea kuridhishwa na mwitikio wa wananchi katika kutumia bidhaa zilizosajiliwa na kuthibitishwa ubora na shirika hilo.

Miongoni mwa bidhaa za vifungashio na vibebeo vilivyokaguliwa ni pamoja na mifuko ya plastiki ya kufungia mikate, maziwa, barafu ,karanga na vingine.

Akizungumza na gazeti na hili mwingoni mwa wiki, Mkaguzi wa TBS, Hellen Mamkwe alisema bidhaa hizo zinasajiliwa na TBS ikiwa ni kutekelezwa takwa mojawapo la Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mzingira (NEMC) kuhusiana na vifungashio vya plastiki.

Alisema mtengenezaji ya vifungashio anatakiwa aweke anuani ya kiwanda chake, aoneshe kwamba vifungashio hivyo ni kwa ajili ya kufungashia bidhaa za chakula na aoneshe kuwa bidhaa hiyo kuwa inaweza kurejereshwa.

Alisema takwa jingine muhimu hi bidhaa hiyo ioneshe kuwa imesajiliwa na kuthibitishwa ubora wake na TBS. Alisema wanachokifanya jijini Mwanza ni kuhakikisha wanawatambua wazalishaji wote wa bidhaa za vifungashio kwa kupita kwenye viwanda mbalimbali vinavyojiusisha na uzalishaji wa bidhaa hizo .

Kwa upande wa usajili wa majengo ya bidhaa za vyakula na vipodozi, Mamkwe alisema wamefanyakazi hiyo Wilaya ya Ilemela na Nyamagana bado kazi hiyo inaendelea.

Alisema katika Wilaya ya Nyamagana wameanza na eneo la Mkuyuni na Kata ya Butimba na kwamba zoezi hilo limekuwa na mwitikio mzuri. Kuhusu mwitikio wa wananchi kuuza bidhaa zilizothibitishwa na TBS, alisema ni mzuri.

Alisema wengi wanajua kwamba wanatakiwa kuuza bidhaa zilizothibitishwa na TBS na zioneshe tarehe ya mwisho wa matumizi na taarifa nyingine muhimu .

Hata hivyo alisema kwenye baadhi ya maduka wamekuta kuna bidhaa ambazo zimeisha muda wake wa matumizi na wameziondoa dukani.

Alitoa mwito mwa wananchi wanapoenda kununua bidhaa wahakikishe wanaangalia tarehe ya mwisho ya matumizi kama haina haipo wasinunue bidhaa hiyo.

Kwa upande wake Afisa Usalama wa Chakula wa TBS, Deus Mlenga alisema kwa sasa kiwango cha uelewa ndani ya jamii kuhusiana na matumizi ya bidhaa zilizosajiliwa na kuthibitishwa nan TBS ni mkubwa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz