Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBS kuongeza ubora wa viwango vya Korosho kwa soko la nje

Kororshooooo TBS kuongeza ubora wa viwango vya Korosho kwa soko la nje

Thu, 16 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) leo Tarehe 16 Septemba, 2021 limeanzisha mkakati wa kuongeza ubora wa viwango vya zao la Korosho pamoja na bidhaa zinazotokana na zao hilo.

Hatua hii inakuja kufuatia uhitaji mkubwa wa zo hilo katika soko la nje jambo ambalo wameona lina tija katika kuongeza pato la taifa.

Katika kufikia maalengo hayo shirika hilo limeanzisha mafunzo kwa wakulima na wajasiriamali wa zao hilo ili kuwaonoa vizuri waweze kupambana na ushindani wa soko la kimataifa.

TBS wanashirikiana na SIDO katika kuhakikisha mpango unafikiwa, kwa kuzingatia maeneo makuu manane ambayo ni kanuni bora za kilimo, viwango bora, teknolojiaa, usajili wa biashara, kanuni bora za usindikaji, vifungashio, upatikanaji wa korosho ghafi, uratibishaji wa wa bidhaa kabla yakusafirisha nje.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live