Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBS kudhibiti wazalishaji wa tofali

Untitled 1 0 Kaimu Mkurugenzi wa TBS akizungumza

Sat, 23 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la viwango nchini Tanzania (TBS) limewakumbusha wazalishaji wa matofali na wasafirishaji wa bidhaa nje ya nchi kuwa TBS ndiyo wenye jukumu la kuweka na kusimamia viwango vya kitaifa hivyo kuhakikisha wanafuata utaratibu na sheria.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya TBS na wasafirishaji wa bidhaa za nje ya nchi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Mhandisi Johaness Maganga amesema kuwa wao wana jukumu la kutoa mafunzo na ushauri viwandani juu ya uzalishaji wa bidhaa bora.

“sisi tunajukumu lingine pia la kupima na kuhakiki vipimo vinavyotumika viwandani pamoja na kuelimisha umma juu ya masuala yote yanayohusu uwekezaji na usimamizi wa viwango pamoja na udhibiti wa ubora wa bidhaa sasa ni nafasi kwenu wazalishaji kushirikiana na watalaamu  wetu ili kuepusha sintofahamu kwenye utekelezaji” alisema Jahaness

Katika hatua nyingine Mhandisi Maganga amesema kuwa TBS itaendelea kuandaa mikutano mbalimbali kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali hapa nchini lengo likiwa ni kujenga uelewa kuhusu umuhimu wa kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango.

Pamoja na hayo wadau walishukuru kwa jinsi ambavyo TBS imetambua umuhimu wakuwa na mkutano huo kwani wameongeza uelewa na waliahidi kufikisha kwa wenzao walioshindwa kufika kutokana na kutingwa na majukumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live