Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TBL yakubali kufuata maelekezo ya Serikali

Bashe Shayiri Kilimo Mhe. Hussein Bashe

Fri, 4 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imewahakikishia wakulima wa shayiri kupata soko la uhakika kwa kuiuzia moja kwa moja Kampuni ya Bia Tanazania TBL .

Akizungumza baada ya kikao chake na viongozi wa TBL kilichohudhuriwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Anthony Mavunde, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amesema wamekutana na viongizi wa TBL kufuatia kauli iliyoitoa hivi karibuni jijini Arusha kuhusu TBL kiingia mikataba ya kununua shayiri moja kwa moja kutoka kwa wakulima

Mhe. Bashe amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 TBL imedhamiria kufanya uwekezaji mkubwa nchini na iliiomba serikali mambo kadhaa ambayo yangeirahishia kampuni hiyo kuwekeza.

Waziri Bashe ameyataja maombi hayo ikiwa ni pamoja na nafuu ya kodi kwa zao la shayiri kama malighafi na kupata ardhi mkoani Dodoma.

Aidha Mhe. Bashe amebainisha kuwa kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Wizara ya Fedha serikali imeikubalia TBL maombi waliyoomba.

Pamoja na kukubaliwa kwa maombi waliyoomba, TBL imekubaliana na serikali kuingia mikataba na wakulima ya kununua tani za shayiri zisizopungua 5,000 hadi 6,000 kwa mwaka kutoka kwa wakulima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live