WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) imetoa wito kwa wawekezaji wa sekta binafsi na Taasisi za Fedha kuwekeza katika miradi ya TBA.
Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 16, Dar es salaam wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na TBA Mkurugenzi wa Miliki TBA, Saidi Mndeme amesema Miradi imegharimu Sh bilioni 69.2 ambayo ni Temeke Kota, Magomeni Kota na Masaki ambayo ilianza Septemba 2021 hadi Septemba 2023 isivyo bahati miradi hiyo haikuweza kukamilika kwa wakati kwakuwa wakala hutegemea ruzuku kutoka serikalini.
“Kwa sasa wakala upo tayari kushirikiana na sekta hizo na kabla ya mwisho wa mwezi huu tutangaza makazi ya nyumba hizi na nyumba zitakazojengwa na sekta binafsi zitatumiwa na wananchi wote.
Majengo haya yalikuwa yanatumia fedha za ndani na sasa serikali imeridhia kushirikisha sekta za fedha na sekta binafsi” amesema Mndeme
Fedha hizo zimeelekezwa kwenye miradi ya uendelezaji wa miliki kwa maana ya ujenzi wa majengo mapya ya serikali na ukarabati wa majengo ya serikali kwa ajili ya utatuzi wa makazi ya wananchi.
Vilevile Mndeme ameishukuru Wizara ya ujenzi na uchukuzi kwa usimamizi wake madhubuti kwa miradi inayoitekeleza kwa weledi wa hali ya juu.