Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TATOA yatoa kero tatu usafirishaji mizigo, DRC, Zambia

CBAAD72F CAE1 4CAA 9A57 4DDD30FAA521.jpeg TATOA yatoa kero tatu usafirishaji mizigo, DRC, Zambia

Sun, 22 Jan 2023 Chanzo: Mwananchi

Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Wamiliki wa Malori na Usafirishaji Tanzania (TATOA), Angelina Ngalula ameshauri taasisi za Serikali zinazohusika na usafirishaji kuwa na sera na sheria zinazolingana ili kuondoa migongano kwa wadau.

Amesema kama suala hilo halitafanyiwa kazi haraka ni wazi kuifungua nchi kutakuwa na kitendawili pamoja na kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ameshaonesha njia ya kuendelea kuitangaza nchi katika nchi mbalimbali duniani.

Akiifafanua changamoto hiyo na zingine leo Januari 21, 2023 kwenye mkutano mkuu wa saba wa mwaka wa chama hicho, Angelina ameeleza kwa sasa watendaji wa taasisi hizo wamekuwa wagumu kukaa pamoja na kuja na mkakati mpya.

“Tunahitaji mfumo mmoja wa kimtandao utakao waunganisha wadau wote wa usafiri pamoja ili tuweze kutatua changamoto ya kutuma taarifa pale bandarini kwa sababu taasisi zilizopo pale ni nyingi zinafanya kazi moja lakini kuna baadhi ya sheria zinapishana,” amesema.

Kuhusu tozo, amesema hakuna usawa, akisema kwa nchi ya Zambia magari ya Tanzania wanatozwa dola 16 za kimarekani ikiwa ni sawa na Sh37,360, wakati Wazambia wakiingiza magari yao nchini wanatozwa dola 10 sawa na Sh23,350.

“Dola sita ni nyingi na ukizingatia Tanzania tunaingiza magari mengi Zambia sasa mambo kama haya ni lazima tukae pamoja na wenzetu tukubaliane tufikie malengo ya pamoja kwakuwa tunategemeana,” amesema Angelina.

Naye Elias Lukumay aliyerithi nafasi ya Angelina baada ya kustaafu, amesisitiza hoja hiyo akisema Tanzania kuna malori Zaidi ya 25,000 yanayofanya shughuli za usafirishaji hivyo kunahitaji zaidi sheria ziboreshwe ili waongeze mengi zaidi.

"Tunahitaji Serikali kuongeza mpaka mwingine wa ziada pale Tunduma, ili hata inapojitokeza changamoto kuwepo na njia mbadala ya kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako mizigo mingi inaelekea huko," amesema.

Amesema kukosekana kwa mpaka mbadala wa Tunduma kunawafanya kutumia siku 60 kusafirisha mizigo kutoka Tanzania kwenda DRC na kuzidiwa na Afrika Kusini wanaotumia siku 30 kwenda na kurudi.

Akijibu hoja hizo, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo, amesema changamoto zote zikizoelezwa serikali itazifanyia kazi na nyingine wameshaanza kuzifanyia.

Chanzo: Mwananchi