Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limekuwa mwenyeji wa mkutano wa nchi wanachama wa Jumuiya wa Maendeleo ya Bahari, ambapo likiweka mikakati ya kulinda maendeleo ya bahari nchini. Akizungumza Agosti 16, katika mkutano huo Mkurugenzi wa Huduma wa TASAC, Moses Mabamba amesema mkutano uliowakutanisha wataalamu zaidi ya 70 kutoka mataifa tofauti, ni kujadili ulinzi wa bahari na kuunga mkono maendeleo yake.
“Tunategemea baada ya siku mbili hizi tutakuja na bangokitita itayowasilishwa kwenye nchi wanachama kwa ajili ya kuona jinsi gani maendeleo ya bahari, hususani kwenye ujenzi wa bandari unavyoweza kufanyika bila kuathiri ikolojia ya bahari,” amesema Mabamba.
Amesema Tanzania kama ambavyo zilivyo nchi nyingine zilizotia sahihi katika mikataba tofauti ya kimataifa inayohusu usimamizi wa masuala ya bahari pamoja na mazingira katika miradi yote ambayo itakuwa ikifanywa na serikali ya awamu ya sita inaangalia kwa kiasi kikubwa jinsi gani mazingira yanavyo simamiwa.
“Kwenye miradi yetu yote wataalamu wetu wapo na wameishauri vizuri serikali na hakuna mradi ambao utatekelezwa kwa kuathiri mazingira kwani miradi yetu yote inafata taratibu,” amesema Mabamba.
Kwa upande wake Lidia Ngugi ambaye ni mkuu wa Ushirikiano wa Teknolojia ya Bahari kwa Afrika (MTCC Africa), ameeleza kwamba umuhimu wa mkutano huu ni kuhakikisha uendelevu wa bandari unafanywa kwa usahihi.
“Natunatumaini baada ya mkutano huu yatasaidia kuendeleza maendeleao ambayo yatasaidia kizazi kijacho katika uendelevu wa bandari” amesema Ngugi
Naye Jaret kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia mambo ya mazingira amesema madhumuni makuu ya mkutano ni kuangalia jinsi gani waneza endeleza maendeleo ya bandari kwa kuzingatia mazingira kwa sababu bandari ni muhimu kwa kuleta maendeleo.