Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TASAC yasaidia wanafunzi usalama majini

A9f03d1665ca572599f7623c46b16a0c TASAC yasaidia wanafunzi usalama majini

Sun, 26 Jun 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SHIRIKA la Uwakala wa Meli nchini (TASAC), limetoa maboya zaidi ya 25 kwa wanafunzi wa shule za msingi Rumuri Kashai na Nyamkazi wanaolazimika kutumia Ziwa Victoria kila siku kwenda shuleni kutoka visiwa vya Msira.

Akizungumza wakati wa kufunga maonesho ya siku ya mahabaria mkoani Kagera, Katibu Tawala wa Mkoa huo Prof. Faustine Kamuzora, ameipongeza TASAC na kusema kuwa pamoja na juhudi hizo serikali imeendelea kuwekeza kwenye ujenzi wa meli, ili kuhakikisha wakazi wa Kanda ya Ziwa wanakuwa na usafiri wa uhakika kwa njia ya maji.

“Niwapongeze kwa juhudi mnazofanya za kuwafikia wananchi, wanapata elimu sahihi na watoto wetu wanapata vifaa vitakavyowasaidia wanapotumia usafiri wa majini.

“Nawaomba pia tuendelee kutoa elimu zaidi, ili kuendelea kuwanusuru na vifo vinavyotokea kutokuwa na vifaa sahihi vya majini,” alisema Prof. Kamuzora.

Aliwataka wananchi na wanafunzi hao kuvitunza vifaa hivyo, ili viweze kudumu kwa muda mrefu, kwani vimenunuliwa kwa kutumia fedha za serikali, huku akisisitiza elimu zaidi kutolewa kwa wakazi wanaosafiri kwenda visiwani, kwani mkoa wa Kagera una visiwa vinavyokaliwa na watu vipatavyo 39, hivyo elimu ya usafiri kuhusu usalama wa maisha yao inahitajika.

Mwenyekiti wa bodi ya TASAC, Musa Mandia alisema wakala pamoja na udhibiti unaendelea kusimamia viwango vya mabaharia, ili kuhakikisha wanapata vyeti vyenye sifa za kuwaruhusu kuajiriwa ndani na nje ya nchi.

Naye Meneja wa Masoko na Elimu kwa Umma, Josephine Bujiku, ambaye alimuwakilisha MKurugenzi Mkuu wa TASAC, alisesema kupitia maonyesho hayo TASAC, imewafikia zaidi ya wananchi 3000 kwa kuwapa elimu ya usalama ili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.

Chanzo: www.habarileo.co.tz