Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TASAC yakusanya bil 87/- mwaka mmoja

Pesa Fedhaddd TASAC yakusanya bil 87/- mwaka mmoja

Wed, 9 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), limekusanya zaidi ya Sh bilioni 87 katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Machi hadi Februari mwaka 2021/2022 ikilinganishwa na mwaka 2020/2021 ambao makusanyo yalikuwa ni Sh bilioni 82.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Kaimu Mkeyenge, wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, jana Dar es Salaam.

Alisema katika kipindi cha mwaka mmoja wamefanikiwa kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuzalisha mabaharia kwa asilimia 100.

Alisema shirika hilo limefanikiwa kuongeza ukusanyaji wa mapato hayo baada ya kuboresha mifumo mbalimbali sambamba na kutoa huduma kwa wakati licha ya kukabiliwa na changamoto ya uchache ya meli kuingia uliosababishwa na janga la Covid-19.

“Shirika limefanikiwa kukusanya mapato na kupata ziada ya shilingi bilioni tano kwa mwaka 2021/2022, katika kipindi kama hiki cha mwaka 2020/2021 tulikuwa tumekusanya shilingi bilioni 82 lakini mpaka sasa kuanzia kipindi cha Machi hadi Februari 2021/2022 shirika limekusanya shilingi bilioni 87,” alisema.

Aidha, alisema shirika limefanikiwa kuongeza idadi ya mabaharia ambao wamekuwa wakiwazalisha kila mwaka kwa zaidi ya asilimia 100 tofauti na takwimu za mwaka 2020/2021. Wameajiriwa katika nchi mbalimbali duniani.

“Tumepima mafanikio ya taasisi kuanzia mwezi Machi hadi Februari mwaka 2020/2021 na Machi hadi Februari 2021/2022, mafanikio ni mengi katika sekta ya uchukuzi hususani usafirishaji kwa njia ya maji,” alisema.

Alisema shirika limekuwa likitekeleza majukumu yake katika kudhibiti shughuli zote za usafirishaji kwa njia ya maji pamoja na masuala ya usalama na ulinzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live