Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TASAC yakoshwa ujenzi bandari ya shehena chafu

Bandari Kavu (600 X 303) TASAC yakoshwa ujenzi bandari ya shehena chafu

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imepongeza jitihada za Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kujenga bandari ya kuhudumia mizigo mchafu eneo la Kisiwa-Mgao, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani hapo.

Pongezi hizo zometolewa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Nahodha Mussa Mandia wakati wa ziara ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na TASAC chini ya usimamizi wa bodi hiyo iliyoanza Novemba 6, mwaka huu.

Pamoja na shughuli nyingine, wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya TASAC walikagua shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na shirika hilo ikiwa ni pamoja na kuwatembelea watoa huduma wanaodhibitiwa na TASAC.

Wajumbe hao walipata fursa ya kutembelea meli za kigeni zinazokuja mkoani Mtwara na kupata taarifa ya vyombo vidogo vinavyokaguliwa na TASAC katika mialo mbalimbali katika ukanda huo.

Ziara hiyo inatarajiwa kuhitimishwa tarehe 11 Novemba, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live