Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TASAC, TPA yajipanga kudhibiti mapato kusini

4d07e0d001bd764611f7486a6a258cb8.jpeg TASAC, TPA yajipanga kudhibiti mapato kusini

Fri, 29 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

“ Tutadhibiti vyombo vinavyoingia na kutoka kwenye bahari katika eneo la Pwani, tusaidiana na TPA (Mamlaka ya Bandari) kudhibiti mapato ya serikali yasipotee, lakini tutashirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha dawa za kulevya, wahamaji haramu na biashara zingine haramu hazipiti Kilwa, “ anaeleza Kaimu Meneja Usajili wa Shirika la Uwakala wa Meli nchini (TASAC), Mhandisi Alfred Waryana

Mhandisi huyo alisema hayo jana mjini Mtwara baada ya kutembelea Bandari ya Mtwara kujionea huduma za mamlaka zinazohusika bandarini lakini pia kujionea shughuli mbalimbali za usafirishaji na kiuchumi zinavyofanyika katika bandari hiyo kubwa zaidi Ukanda wa Kusini mwa nchi.

Mhandisi huyo alisema, “Tunaamini tunachangamoto kubwa kwenye udhibiti wa vyombo vya majini. Usalama unaanza bandari, lakini tunaona sehemu nyingi bado hazijawa rasmi hivyo tuna kazi ya kubadili hii hali kwa kuhakikisha miundombinu inayokuwepo inaruhusu ukusanyaji wa mapato ulio na faida.”

Kiongozi huyo akashauri menejimenti ziwepo kwenye bandari bubu, mialo na gati zisizokuwa rasmi ili vyombo vyote vya majini visajiliwe na udhibiti uwepo ili vinapokuwa majini vinakuwa mali na abiria wanakuwa salama.

Kwa upande wake, Meneja wa TPA Kanda ya Kusini, Mhandisi Juma Kijavara alisema kuwa licha ya kuwepo maendeleo makubwa kwenye bandari za ukanda wa Kusini na kwamba Serikali inaendelea kuboresha ili ijikusanyie vyema mapato.

“ Tuna na bandari kama hii ya Mtwara na nyinginezo kule Lindi ambazo zimeboreshwa na zinaiongezea Serikali kipato. Hata sasa Serikali itarasimisha zingine ili ziongeze makusanyo sambamba na kuboresha huduma kwa wananchi wanaosafiri na kufanya biashara mbalimbali.

“ Lengo la Serikali ni zuri na tunawaita wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali wa bidhaa za majini au hata nyinginezo watumie bandari rasmi ili waongezee mapato Serikali na pia kwa ajili ya usalama wa bidhaa zao,” alisema na kuongeza;

“ Mfanyabiashara yoyote mwenye mzigo mkubwa na anataka unafuu wa bei afike kwenye bandari zetu zilizorasmi, Serikali inatoa unafuu wa bei lakini pia inawezesha mazingira mazuri ili kukuza uchumi wa nchi na pia wa mtu mmoja mmoja.”

Chanzo: habarileo.co.tz