Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TASAC: Leteni taarifa vivuko vinavyozidisha abiria

Kivuko Kujaza TASAC TASAC: Leteni taarifa vivuko vinavyozidisha abiria

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limawataka wananchi kutoa taarifa za vivuko vinavyozidisha abiria ili hatua zichukuliwa.

Rai hiyo imetolewa jana Jumatano Juni 8, 2022 na Ofisa usimamizi na udhibiti wa usafiri kwa njia ya maji, Gabriel Manase wakati semina ya kuelimisha wahariri na waandishi wa vyombo vya habari juu ya shughuli za Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) na sheria zinazosimami sekta ya maji iliyofanyika Bagamoyo mkoani Pwani.

Manase amesema kuwa sheria na kanuni zinabainisha adhabu kwa vyombo vya majini vikiwamo vivuko ambavyo vinabeba abiria zaidi ya uwezo.

Hata hivyo, Manase amesema kuwa ingawa kanuni na sheria zinawataka watoa huduma kuandikisha abiria wanoingia kwenye vyombo hivyo lakini sheria hizo zinaelekeza kuwa kinachohitajika kwa vivuko vya safari fupi ni taarifa ya idadi ya wanaoingia kwenye vyombo hivyo.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu vivuko vya Feri-Kigamboni vinavyodaiwa kubeba abiria wengi, Manase amesema vivuko hivyo vinafuata utaratibu kwa kuwa abiria wakiingia wanahesabiwa kupitia mfumo wa ukatishaji teketi.

'Hata pale Feri (Dar es Salaam) kuna mfumo wa kutambua idadi ya abiria wanaoingia kupitia zile kadi na wanaokata tiketi, ila leteni taarifa za vivuko vinavyozidisha abiria tutachukua hatua" amesema Manase ambaye ni baharia

Amebainisha kuwa kuona kwa macho kuwa chombo kimezidisha abiria inaweza isilete uhalisia wa kama chombo hicho kimezidi uwezo wake.

"Tuna utaalamu wetu wa kutambua kama chombo kimezidisha uwezo wake, inaweza ikawa kuwekwa alama ambayo ikipita kwenye alama hiyo wataalamu watatambua kama mzigo umezidi"

"Mnaweza mkaona watu ni wengi lakini bado ikawa haijafikia ukomo wa uwezo unaotakiwa" amesema baharia Manase.

MV Kazi yasimamishwa

Katika kudhibiti na kuhakikisha usalama wa abiria Manase amesema shirika hill likibaini kuwa chombo hakiko salama wanakisimamisha ili kifanyiwe marekebisho.`

Amesema kivuko cha MV Kazi kilichokuwa kikivusha abiria Feri-Kigamboni  kimesimamishwa baana ya kugundolika kuwa hakipo salama kufanya lazi.

"MV Kazi tulibaini kuwa hakifanyi kazi kama inavyotakiwa,  ndio maana kikasimamishwa"

Kivuko hicho ambacho kilikuwa  ni miongoni mwa vivuko vinavyotumika Feri-Kigamboni kilisimamishwa miezi miwili iliyopita ili kifanhiwe ukarabati.

Hata hivyo, Manase ametoa tahadhari kwa vyombo vidogo vikiwamo mitumbwi inayofanya kazi za kuvusha abiria hasa kwa Dar es Salaam kuacha kwa kuwa haviruhusiwi kufanya shughuli hiyo.

 Changamoto

Akizungumumzia changamoto zinazolikabili shirika hilo, Mkurugenzi wa Huduma wa TASAC, Rajab Mabamba amesema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni watoa baadhi ya watoa huduma kutofuata masharti yanayoelekezwa na leseni husika.

"Changamoto kubwa ni baadhi ya watoa huduma hawafuati masharti ya uanzishaji wa vyombo vyao" amesema

Mabamba ametaja changamoto nyingine kuwa ni uelewa mdogo wa jamii juu ya majukumu ya TASAC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live