Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TARURA yakagua miradi, yatoa maagizo

TARURA MRADIIII TARURA yakagua miradi, yatoa maagizo

Thu, 14 Jul 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) nchini Tanzania kwa kushirikiana na bodi wameendelea na ziara ya kutembelea miradi mbalimbali, ikiwemo inayofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya (EU).  

Aidha, Bodi ya Tarura imetoa maagizo ya kuwekwa lami mabega ya barabara ili kuwawezesha wanafunzi pamoja na shule zilizopo jirani kuvuka kwa usalama.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua barabara ya Masebe Dispensari hadi Bugoba kibaoni, Mtendaji Mkuu wa Tarura, Victor Seff alisema, barabara hizo zenye urefu wa kilomita tano zimeshakamilika na zipo kwenye kipindi cha matazamio.

Alisema kiasi cha Sh 2.1 bilioni zilitumika katika ujenzi wa barabara hiyo, ambapo mwaka mmoja uliopita bodi hiyo ilipita na kutoa maagizo, ikiwemo kuweka lami mabega ya barabara.

“Ni vizuri kuwekwe lami kwa usalama wa wanafunzi pamoja na shule zilizopo jirani, lakini katikati palitakiwa kuwa na kivuko, ili wanafunzi waweze kuvuka pale kwa uslama wasije kugongwa na magari,” alisema Seff.

“Alama za kuvuka zimewekwa lakini haziendi moja kwa moja hadi shuleni, kwahiyo agizo lingine ambalo bodi ilitoa ni kwamba, wajenge njia ya miguu ili wanafunzi wakivuka wafike shulemi moja kwa moja bila kutembea kwa kufuata barabara,”alisema.

Advertisement Mkazi wa Mpuguso Rungwe, Maria Kasege ameshukuru Serikali kwa kuwajengea barabara kwa kuwa itawapunguzia makali, ikiwemo adha waliyokuwa wanaipata ya kubeba ndizi kichwani na kutembea umbali mrefu.

“Tulikuwa tukibeba ndizi kutoka chini na kutembea hadi sokoni, saivi tunashukuru kwa barabara hii hata pikipiki zinatusaidia kubeba, pamoja na kutusaidia kujega vizuri tulikuwa tunaomba mtusaidie kuweka matuta kwaajili ya watoto,” alisema Kasege.

Alibainisha pikipiki na magari zimekuwa zikienda mwendo mkali, hivyo kusababisha hatari ya watoto wanaosoma shule ya Masebe, yatawekwa matuta angalau wale wenye magari watanguza mwendo.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz