Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TARI yazindua kituo mahiri cha usambazaji teknolojia za kisasa za kilimo mkoani Morogoro

B1aa6b66628b181d3d88cf8d1fba3bac TARI yazindua kituo mahiri cha usambazaji teknolojia za kisasa za kilimo mkoani Morogoro

Sat, 19 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Taasisi ya utafiri wa Kilimo Tanzania TARI imezindua kituo mahili cha usambazaji wa teknolojia za kisasa za kilimo mkoani hapa, kituo hicho kinatarajiwa kutoa mafunzo kwa wakulima kwa mwaka mzima ili kuongeza tija na uzalishaji.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kituo hicho mkurugenzi Mkuu wa TARI Dk. Geofrey Mkamilo alisema kuwa kituo hicho kitakuwa kikitoa mafunzo mwaka mzima na pia kitakuwa na wataalamu mbalimbali wa kilimo wakiwemo watafiti na wataalamu wa huduma za ugani.

Dk. Mkamilo alisema Taasisi hiyo iko tayari kuhakikisha inaleta mapinduzi ya kilimo na kuhamasisha wakulima kuachana na kilimo mazoea walichokuwa wanalima mababu na mabibi.

Alisema kuwa katika kuboresha kilimo na kuongeza uzalishaji nchini TARI imekuwa ikifanya kazi na taasisi nyingine ikiwemo taasisi ya udhibiti wa ubora wa mbegu TOSCI,Wakala wa Mbegu ASA na makampuni mengine ya uzalishaji na usambazaji wa mbegu.

Akizungumzia majukumu ya TARI Dk. Mkamilo alisema kuwa inaratibu shughuli za utafiti na kuhamasisha matumizi ya teknolojia za kilimo na ubunifu kwa lengo la kuongeza tija.

Naye Mkurugenzi wa kituo cha utafiti TARI Mlingano Dk. Catherine Senkolo alishauri wakulima wa migomba kulima mazao ya mikundekumbe kwenye shamba la migomba ili kutunza unyevunyevu na pia kutengeneza mbolea ya samadi.

Alisema kuwa mikundekunde kwenye shamba la migomba pia linasaidia kuondoa ugonjwa wa minyoo kwenye migomba ambao umekuwa ukisababisha uzalishaji kupungua.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mathayo Masele aliwataka maafisa ugani kuituma taaluma yao kivitendo ikiwa ni pamoja na kuwa na mashamba darasa katika maeneo waliyopo ili wakulima waweze kupata elimu na maarifa ya kilimo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz