Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TARI yahimiza wakulima wa mihogo kulima kibiashara.

TARI Ed.jpeg TARI yahimiza wakulima wa mihogo kulima kibiashara.

Tue, 25 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Ushauri huo umetolewa na Mtafiti wa Mazao ya Mihogo na Viazi Vitamu, Festo Masisila, wakati akitoa ufafanuzi kwa wakulima kuzingatia mafunzo yanayotolewa na wataalam kwa mfumo wa shamba darasa kwa ajili ya kuwasaidia wakulima waweze kujifunza kwa vitendo.

Masisila, amesema wameweka mashamba darasa katika Mkoa wa Lindi, Mtwara na Ruvuma, na katika mashamba hayo wamepanda mbegu nane tofauti zenye kuvumilia ukame, huku zikiwa kinzani na magonjwa na wadudu waharibifu kwa ajili ya  kutoa elimu kwa wakulima wa mikoa hiyo.

Amesema zao kuu la chakula kwa Mkoa wa Lindi na Mtwara ni muhogo, na kwamba wakulima wa maeneo hayo wanapaswa wajielekeze kulifanya zao hilo kuwa la biashara zaidi kwa kuwa na mazao bora.

“Wakulima wasiridhike na kulifanya zao la muhogo kuwa chakula peke yake, wajielekeze pia kulifanya liwe la kibiashara na hili litafanikiwa kwa kutumia mbegu bora na kuachana na mbegu zile zisizokuwa na matokeo ya uhakika, kwani kuna soko kubwa sana la mihogo ndani na nje ya nchi tutumie fursa hii kulishika soko”amesema Masisila.

Mmoja wa wakulima hao Ashura Rwaba, amesema wamekuwa wakihofia soko la bidhaa hiyo ndani na nje ya nchi kabla ya kupewa uhakika wa soko la mihogo kutoka kwa wataalam wa TARI.

"Changamoto ni kubwa kwenye zao la muhogo na tumekuwa na mbegu nyingi tunazotumia bila kuwashirikisha wataalam na hazikuwa na tija kwetu,lakini ujio wa mbegu hizi bora tuna uhakika wa kupata mavuno ya kutosha na tutaingia kwenye biashara” amesema Rwaba.

Chanzo: ippmedia.com